Jana katika Monday Night Football,Timu ya Arsenal iliambulia kipigo cha bao 1 - 0 kutoka kwa timu ya Swansea
City katika mchezo wa ligi kuu England uliopigwa katika dimba la Emilates,na kuifanya Swansea City kuwa na hatua moja tu nyuma Southampton katika kinyang'anyiro cha kucheza michuano ya Europa League.
Lakini Licha ya mchezo huo wa jana usiku,kuna timu ambazo tayari zimeshakwisha kushuka daraja katika Ligi ya England,kabla ya ligi hiyo kumalizika rasmi,na moja wapo ya timu hizo ni Queens Park Rangers(QPR),ambapo imefahamika kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Chris Ramsey atafanya kazi kwa muda wote atakao kuwepo, licha ya klabu hiyo kushuka daraja kutoka Ligi Kuu.
Hilo limethibitishwa baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Manchester City siku ya Jumapili, wakati Ramsey alihojiwa baada ya mchezo, kuwa kama bado alikuwa na tumaini kuifundisha timu hiyo msimu ujao.
Alipoulizwa kama anataka kukaa katika dimba Loftus Road, Ramsey alijibu: "Ndiyo, kwani klabu hiyo iko katika moyo wake na anataka.. kuwa hapo. "
Bodi ya klabu QPR inafahamu kuchagiliwa kwa Chris Ramsey, ambaye alichukua madaraka baada ya Harry Redknapp kuondoka ghafla mwezi Februari.
Ramsey awali aliteuliwa kuwa Mkuu wa Maendeleo ya mchezaji na Meneja wa Chuo katika klabu ya QPR mwezi Novemba 2014 na amefanikiwa kushinda mechi mbili tu kati ya mechi zake 13 akiwa na timu ya kwanza.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments