1.Utasikikia taarifa juu ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kuingia kambini kesho jumatano katika
hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa AFCON.
Msemaji wa shirikisho la soka nchi Baraka Kizuguto anataja wachezaji walioitwa.
2.WEKUNDU wa Msimbazi, Simba wameanza harakati za kuwabakisha nyota wake waliomaliza mikataba baada ya kumsainisha mkataba kiungo wake mchezeshaji, Said Ndemla,ni miaka mingapi?
3.YANGA SC nayo imeendelea na usajili wa wachezaji wapya kuelekea msimu ujao, na leo wamesajili wachezaji wawili makao makuu ya klabu, Jangwani.
4.Taarifa nyingine ni Mashindano ya mpira wa kikapu ya majiji yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam na kumalizika siku ya Jumapili Tarehe 30 mwezi huu.
Raisi wa kamati ya mpira wa kikapu majiji Ndugu Saimon Msofe pamoja na wachezaji wanaelezea maandalizi ya mashindano hayo.
SIKILIZA HAPA.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

0 Comments