Ticker

6/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS:CAF YAIPA TANZANIA UENYEJI FAINALI ZA U17

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May .26,2015 SAA 04:57 USIKU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika -CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika
ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.

Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi. 

Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.

TFF inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na Mh. Fennela Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments