kwa mujibu wa vyanzo vya habari mbalimbali Barani Ulaya ikiwemo Sky,vinasema kuwa klabu ya Liverpool watatafakari
msimu uliomalizika, lakini si kuzingatia kumfukuza meneja Brendan Rodgers majira haya.
The Reds, ambao walimaliza wa pili katika msimu wa 2013/2014, na kumalizika msimu huu kwa kipigo cha mabao 6-1 katika mikono ya Stoke Jumamosi - na hivyo kusababisha uvumi kuwa kocha Rodgers huonda akaonyeshwa mlango wa kutokea na wamiliki wa klabu ya Liverpool.
Lakini pamoja na kipigo hiko kizito alichopata kwenye Uwanja wa Britannia,Liverpool wamemaliza katika nafasi ya sita-Ligi Kuu, na vyanzo katika klabu hiyo wamependekeza kufanwya mapitio ya msimu uliomalizika - ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Juni - na kuacha kuangalia swala la meneja mpya katika klabu hiyo Liverpool.
Katika mchezo ambao Steven Gerrard aliaga klabu hiyo kwa kufunga bao la pekee la kufutia machozi, Rodgers alisema: "Mara zote nasema kwamba kama wamiliki wanataka niende, basi mimi nitaenda, Ni rahisi kama havyo".
"Lakini bado najisikia nimefanya mengi ya klabu . Mengi yametokea mwaka huu ambao umefanya kazi kuwa ngumu, lakini naelewa kabisa".
kocha Brendan Rodgers pia amesema kuwa kumaliza katika nafasi ya Sita si mahali ambapo walistahili,lakini pia amekiri kuwa ni wazi ukosefu wa Mabao katika msimu uliomalizika pia umechangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kufanya vizuri kwa timu hiyo.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments