Ticker

6/recent/ticker-posts

STARS YAWASILI KINYONGE DAR(PICHA)

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May .23,2015 SAA 12:23 JIONI
Displaying thumb_IMG_1607_1024.jpg
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasii salama leo alfajiri ikitokea nchini Afrika Kusini ilipokua ikishiriki
michuano ya Kombe la Cosafa, baada ya kutolewa katika hatu ya awali ya makundi.

Stars ambayo jana jioni ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho baada ya kufungwa bao 1 - 0, imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote mitatu ya kundi B, baada ya kufungwa na Swaziland, Madagascar na Lesotho.
Displaying thumb_IMG_1601_1024.jpg
Displaying thumb_IMG_1602_1024.jpg
Displaying thumb_IMG_1603_1024.jpg
Displaying thumb_IMG_1604_1024.jpg
Mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij alisema amesikitishwa na matokeo ya timu yake katika hatua hiyo ya awali baada ya kupoteza michezo yote mitatu.

Nooij alisema, mpira wa miguu umebadilika kwani matarajio yake yamekua tofauti, kwani kiwango walivyoonyesha wapinzani wake katika kundi B vimemstajaabisha.

“Mpira wa sasa hautazami nani yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na matarajio ya kufanya vizuri katika michuano hii lakini baada ya dakika ya 90 za kila mchezo matokeo hayakua mazuri kwetu” alisema Nooij”

Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda nacho Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Taifa Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el Arab jijini Alexandria.

ANGALIA PICHA ZA MCHEZO
Displaying thumb_IMG_1617_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1616_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1625_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1624_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1622_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1640_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1656_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1665_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1672_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1690_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_1687_1024.jpg
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments