Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA 8 - 0 COASTAL UNION :ANGALI PICHA JINSI YANGA ILIVYOIANGAMIZA COASTAL UNION UWANJA WA TAIFA (PICHA)

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.APRIL .8,2015 SAA 02:00 USIKU

Yanga Sc imejisogeza karibu kabisa katika mbio za kunyakuwa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara,baada ya hii Leo kuitandika
Coastal Union Kipigo cha mbwa mwizi cha Mabao 8 -0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa Jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ambao Yanga walitawala mchezo wote,Amissi Tambwe alifanikiwa kuondoka na mpira baada ya kufunga mabao manne peke yake.

Kwa ujumla mabao ya yanga yalifungwa na Amissi Tambwe dakika ya 10 kipindi cha kwanza,na dakika ya 23 Saimon Msuva Alifunga bao la pili,Juma Abdul aliachia shuti kali dakika chache kabla ya kwenda mapumziko na Amissi Tamwe akalisindikiza nyavuni na kuiandikia Yanga bao la 3,mpira ukaenda mapumziko kwa Yanga ikiwa inaongoza kwa mabao 3 - 0.
Kikosi cha kwanza cha Yanga
Kikosi cha kwanza cha Coastal Union

Mabao ya kipindi cha pili ya Yanga,Bao la nne lilifungwa na Amissi Tambwe dakika ya 3 ya kipindi hiko, na katika dakika ya 5 ya kipindi cha pili Kpah Sherman aliiandikia Yanga bao la  tano,Saimon Msuva alifunga bao la sita dakika ya 43 kipindi cha pili na Salum Telela aliifungia Yanga bao la 7 dakika moja baada ya bao la sita.

Na Amissi Tambwe ndiye shujaa wa mchezo huo kwa kumalizia bao la 8 la klabu ya Yanga katika dakika ya mwisho kabisa ya mwamuzi Simon Mbelwa kutoka Pwani,na kukamilisha mchezo huo kwa klabu ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 8 - 0 dhidi ya timu ya Coastal union inayoongozwa na kocha wa muda Jamuhuli Kihwelo.

ANGALIA PICHA ZA MCHEZO











































YOUNG AFRICANS.

GK.1.Ally Mustafa,12.Juma Abdul,3.Oscar Joshua,23.Nadir Haroub,5.Kelvin Yondani.6.Mbuyu Twite,2.Salum Telela,8.Haruna Niyonzima,19.Amissi Tambwe,9.Kpah Sherman,27.Saimon Msuva.

Substitutes:
GK.30,Deogratius Munish,4.Rajab Zahir,15.Pato Ngonyani,26.Hassan Dilunga,16.Nizar Khalfan,28.Edward Charles.
Technical Bench
1.Hans Van Pluijm (HOLL)(COACH),2.Chalses Boniface (ASS/COACH),3.Juma Pondamali,(ASS/COACH),4.Suphian Juma(Docter)5.Jacob Onyango(Physio),6.Hafidh Saleh(Maneger),Mahmoud Omar(Kitman)

COASTAL UNION
GK,1.Bakari Fikirini,22.Juma Hamad.15.Mfuko Abdalla,5.Chuma Yusuf,6.Mtama Bakari,24.Hamoud Abdulhalim,13.Mohamed Ally,11.Yahya Ayoub,29.Rajab Mohamed,27.Ike Bright,21.Salim Rama.
Substitutes:
GK.30.Hassan Shaban,19.Rashid Sabri,25.Shekuwe Mohamed,28.Juma Mtenje,3.Mosha Tumain,10.Mtindi Mohamed,17.Athuman Abassi.
Technical Bench
Coach:Jamuhuri Kihwelo,Doctar:Francis Mganga,Meneger:Faraji Mkapa,Kit Man:Mohamed Rajab.

Match Comm:Jumanne Shengelo(Mwanza)
Referee:Simon Mbelwa (Pwani)
1st Asst:Milambo Tshikungu
2ndAsst:Robert Luhemeja (Mwanza)
4th Official:HELLEN Mduma (DSM)

PROTOCAL:RAPHAEL MATOLA
TFF(FIFA)SECURITY OFFICER:SSP JONES MAHANGA
TFF MEDIA OFFFICER:BARAKA KIZUGUTO

SUPERVISOR:WILFRED KIDAO

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments