Timu ya Yanga Sc imejihakikishia ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa asilimia 90 baada ya kuitungua mabao 5 -0 timu ya Ruvu
Shooting,katika mchezo uliopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Shooting,katika mchezo uliopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga na Ruvu Shooting zote ziliiingia Uwanjani zikiwa na lengo la kupata Alama Tatu,lakini kikosi cha Yanga kilionekana kuimarika zaidi katika mchezo huo wa Ligi kuu Tanzania bara.
Yanga sasa imetimiza alama 52,baada ya kucheza mechi 23 na sasa inahitaji alama tatu katika mechi tatu zilizobaki ili kufikisha alama 55 ambazo aziwezi kufikiwa na Azam Fc ambao ni mabingwa watetezi.
Bao la kwanza la Yanga hii leo yalifungwa na Simon Msuva dakika ya 13 kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi safi ya Niyonzima.
Dk 23, Kpah Sherman aliunganisha vizuri pasi na kuifungia Yanga bao la pili.
![]() |
| Kikosi cha Ruvu Shooting kilichoanza hii leo |
![]() |
| Kikosi cha Yanga Kilichoanza hii leo |
Dk 45, Msuva alifunga bao la tatu la Yanga, na la pili kwake leo na la 16 kwake msimu huu.
Dk 58, Tambwe aliifungia Yanga bao la nne baada ya mabeki wa Ruvu kujichanganya na yeye akamalizia kwa ufundi mkubwa,na hilo ni bao lake la 11 msimu huu.
Bao la tano la Yanga lilifungwa Dk 67 na Kpah Sherman kwa kichwa akiiwahi krosi ya Abdul Juma.
ANGALIA PICHA
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .








































0 Comments