Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:ANGALIA SIMBA ILIYOIFUMUA MGAMBO SHOOTING TAIFA,OKWI APIGA HAT-TRICK

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.APRIL .18,2015 SAA 02:45 USIKU

Simba Sc imeibuka na ushindi mzito wa mabao 4 - 0 katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara Dhidi ya Mgambo Shooting,mchezo
uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mshambuliaji wa Simba Emannuel Okwi ndiye aliyeibuka Shujaa katika mchezo huo baada ya kufunga mabao matatu peke yake (Hat -trick) na kuondoka na mpira mara baada ya mechi kuisha.


Bao la kwanza la Emanuel okwi lilipatikana katika dakika ya 8  baada ya kuunganisha krosi safi ya Kesssy aliyegongeana Singano.

Dakika ya 15, Ramahani Singano 'Messi' aliifungia Simba bao la pili kwa mkwaju wa adhabu, uliojaa moja kwa moja wavuni.

Katika Dakika ya 41 Okwi tena akaifungia Simba bao la tatu baada ya mabeki Mgambo kujichanganya na yeye kumtoka mmoja wao kabla ya kufunga kwa shuti kali.Mpira ukaenda mapumziko kwa Simba ikiwa mbele kwa mabao 3 -0.




 Kipindi cha pili kulikuwa na mvua iliyonyesha,na katika dakika ya 51 Okwi alifunga bao la nne la Simba baada ya kuwachambua mabeki wa Mgambo na kuuachia mpira uende wavuni,na mpira mpaka unamalizika Simba 4 - 0 Mgambo Shooting.




KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments