Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:HIVI NDIVYO YANGA WALIVYOTOANA JASHO NA ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.APRIL .18,2015 SAA 02:20 USIKU

Klabu ya Yanga Sc hii leo imeshindwa kuutumia vema uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam,baada ya kulazimishwa
sare ya bao 1 - 1 na timu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Bao la Yanga lilifungwa dakika ya tatu 3 tu ya mchezo huo kwa penalti na Nahodha Nadir Haroub "Cannavaro" baada ya Simon Msuva kuangushwa katika eneo la hatari,na hadi mapumziko tumu hizo zilikuwa zimefungana bao 1 - 1.



Katika kipindi cha pili ndani ya dakika ya pili tu,mchezaji wa Etoile du Sahel  Ben Amour Amine alifunga bao  la kusawazisha baada ya kupiga shuti kali la chini lililomshinda kipa Barthez na kutinga wavuni.Mchezo ukamalizika kwa timu hizo kufungana bao 1 - 1.


Yanga sasa katika mchezo wa marudiano inahitaji ushindi au sare ya kuanzia 2 - 2 ili kuweza kuvuka kizingiti na kuweza kucheza hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho.

ANGALIA PICHA ZA MCHEZO






































KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments