Siku ya jana Jumatatu gazeti la Daily Mirror liliripoti kuwa bosi wa Liverpool Brendan Rodgers katika mkutano na
wachezaji,aliwashtaki wachezaji wake kadhaa kuwa "hawachezi kwa ajili yake na timu",kufuatia kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Arsenal siku ya jumamosi.
Lakini bosi huyo wa klabu hiyo amekanusha ripoti hizo za kuwa na mgogoro katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo siku ya Jumapili, baada ya matokeo hayo mabaya ya kushindwa na klabu ya Arsenal.
Mara baada ya taarifa hizo kutoka Jumatatu,siku hiyo hiyo asubuhi, Rodgers alizungumza na vyombo vya habari,katika mkutano wa kabla ya mechi ya Jumatano usiku ya robo fainali ya marudiano ya Kombe la FA na Blackburn na alipoulizwa kuhusu kama ni kweli wachezaji wana mgogoro naye,Brendan Rodgers aliruka kimanga taarifa hizo.
"Tumefanya mikutano mingi kuangazia makosa yetu,na hakuna tofauti na kikosi tuna mikutano kila mwaka. Mikutano ile imetusaidia kupona kutokana na mwanzo mbaya,"
"Kweli kulikuwa hamna kitu kikiendelea,tulikuwa tunachambua utendaji tu, tunachambua ambapo tupo, na kisha kufikilia mbele na wachezaji.tuna michezo saba mbele na robo fainali ya Kombe la FA malengo yetu yako wazi kufikia kati ya sasa na mwisho wa msimu. Ni bahati mbaya tu kitu kingine kikitokea"alisema
kauli hiyo wa Rodgers inakuja siku chache baada ya kujibu pia mustakabali wa Raheem Sterling ambaye alizungumza na vyombo vya habari bila ruhusa na kudai hata saini mkataba mpya,lakini Brendan Rodgers ana matumaini kuwa swala la mkataba mpya wa Raheem Sterling na Liverpool utatatuliwa katika majira ya joto.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments