Ticker

6/recent/ticker-posts

ROBERTO DI MATTEO AMEYASEMA HAYA JUU YA TAARIFA ZA MGOGORO KATIKA KLABU YA REAL MADRID KUELEKEA MECHI YA LEO

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.March.10,2015 SAA 08:10 USIKU
Roberto Di Matteo: Won the Champions League with Chelsea in 2012
Roberto Di Matteo amekanusha kuwa timu yake ya Schalke 04 ambao wanakutana na Real Madrid katika mchezo wa
marudiano,kuwa wao wana angalia kama wataweza kugeuza matokeo ya mabao 2-0 siku ya leo Jumanne usiku katika hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa,baada ya taarifa kuwepo kuwa timu ya Real Madrid wana mgogoro.

Real Madrid iliwapiga Schalke kwa jumla ya mabao 9-2 katika harakati zao za  kushinda Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 10 msimu uliopita, lakini wamekuwa na mashaka hivi karibuni katika La Liga.

Vijana hao wa Carlo Ancelotti  wamepigwa kwa mara ya nne katika michezo 14 mwaka 2015,Athletic Bilbao siku ya Jumamosi ikapanda katika msimamo wa La Liga unaoongozwa na Barcelona wanaopishana alama moja na Real Madrid.

"Siamini kama Real Madrid wako katika mgogoro, Natumaini vyombo vya habari viko sawa kwamba washambuliaji wao hawako katika fomu nzuri. "Tutahitaji kidogo pia kuwa na bahati  kesho usiku(leo) na kupata matokeo mazuri.."

"Mchezo wa Jumamosi ulikuwa tofauti. ulikuwa ni mchezo wa nyumbani kwa Bilbao, ambao ni timu kali sana, na hawakuweza kuwaruhusu Real Madrid kuwashambulia. Kesho (leo)wao watacheza mbele ya mashabiki wao nyumbani na nadhani itakuwa ni tofauti".alisema Roberto Di Matteo

22:45
FC Porto
Basel
22:45
Real Madrid
Schalke 04
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .


Post a Comment

0 Comments