Meneja wa Manchester United Louis van Gaal anasisitiza kuwa hana majuto kwa kumuuza katika klabu ya Arsenal.
mshindi wa mechi ya Kombe la FA Danny Welbeck na kumsajili Radamel Falcao msimu uliopita.
Welbeck alijiunga na academy ya United akiwa na umri wa miaka nane lakini aliuzwa na Van Gaal Septemba kupisha usajili wa Falcao.
Wakati Mchezaji huyo raia wa Colombia akifanya jitihada kwa klabu hiyo tangu ahamie Old Trafford, Danny Welbeck aliwakumbusha mashabiki wa United sifa zake usiku wa kuamkika leo, kwa bao la ushindi katika ushindi wa Arsenal mabao 2-1 katika robo fainali ya Kombe la FA.
Arsenal imetinga nusu fainali ya kombe hilo,huku United ikiyaaga mashindano hayo,na Louis van Gaal Alipoulizwa kama alikuwa na majuto yoyote juu ya biashara Welbeck kwa Falcao kuchafuka, Van Gaal alisema: "Yeye (Falcao) amefunga mabao manne, amesaidia mara tatu au nne na anahamasisha wachezaji wengine, kwaiyo ana nyanja kitaaluma. Lakini kwa sasa ni rahisi kwa wewe kusema hivyo, na una furaha kusema hivyo. "
mshindi wa mechi ya Kombe la FA Danny Welbeck na kumsajili Radamel Falcao msimu uliopita.
Lakini Louis van Gaal ameikosoa timu yake ya Manchester United kwa kushindwa kujilinda katika mchezo wao wa Kombe la FA baada ya kufungwa na Arsenal.
"Nadhani inasikitisha sana, wakati unapompa ushindi mpinzani wako," . "ikiwa unapoteza mchezo kwa sababu ya upinzani, unapoteza kwa sababu ya wewe mwenyewe".
"Wachezaji wanasikitisha sana kwa sababu wanajua kwamba inaweza kuwa tofauti. Mechi inaamulia kwa magoli na unaweza kuona bao la pili, lilikuwa ni makosa, tulitoa pasi ya mbali. mtu ambaye alifanya hivyo alikuwa mtu muhimu wa timu yangu, na pia kwangu inasikitisha sana. "
Van Gaal pia anakubali Angel Di Maria alikuwa na makosa kwa kugusa mwamuzi,
Angel Di Maria alipewa kadi ya njano baada ya kuonekana akajiangusha,jambo ambalo mchezaji huyo hakukubaliana nalo, na kwenda kuvuta shati la mwamuzi Michael Oliver ,ndipo alipopewa kadi nyekundu.van Gaal anakubali kuwa Angel Di Maria alikuwa na makosa kwa kugusa mwamuzi.
"Nadhani alimgusa mwamuzi na hivyo ni makosa katika kila nchi, hivyo hakuna msamaha," alisema Van Gaal.
"Nchini Hispania yeye anajua kwamba haitakiwi kumgusa mwamuzi,lakini kudhibiti hisia zako si rahisi sana katika mechi kama hii.Tayari Niliongea nao, na wanajua maoni yangu kabla ya mechi,kwani najua aina hii ya mechi,kupata kadi nyekundu ni rahisi"alifafanua Louis van Gaal
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments