Ticker

6/recent/ticker-posts

ANACHOKIAMINI ARSENE WENGER JUU YA MECHI DHIDI YA TIMU YAKE YA ZAMANI

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.March.17,2015 SAA 09:20 USIKU
Arsene Wenger: Says confidence is key for Arsenal to progress
Arsene Wenger Anasema kujiamini ni muhimu kwa klabu ya Arsenal kwa maendeleo yao 
Meneja wa klabu ya Arsenal,Arsene Wenger,amesema klabu hiyo ina haja ya kuamini kuwa wanaweza kuwafunga
Monaco,ikiwa ni kama  hoja kuerekea mchezo wao wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa.

Endapo Arsenal itafanikiwa hii leo,itaandika upya vitabu vya historia kwa kuwa timu ya kwanza kufuzu kwa kufunga bao zaidi ya moja katika hatua hii, kufuatia kufungwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza.

Arsenal, ingawa, hawajawahi kupoteza mchezo nchini Ufaransa, na Wenger haoni sababu ya kwa nini timu yake, haiwezi kukusanya nguvu, ili kuendelea na michezo hiyo ya kimataifa.

"hakika Monaco iko katika nafasi imara sana,lakini tunataka kuonyesha kila kitu kwa kucheza vizuri uwanjani. Kama sisi hatukuamini kama tunaweza kufanya hivyo, basi tusingekuwa hapa".
"Ki Takwimu wako juu yetu kwa matokeo katika mechi ya kwanza dhidi yetu.. tunafahamu kuhusu hilo.
"Lakini bila kujali jinsi ya ukubwa kwa asilimia (nafasi) ni, tutaonesha kila kitu kabisa na kufanya eakwimu zionekane za uongo, tuna uzoefu,tuna  hamu na imani kuwa tunaweza kufanya hivyo"
Wenger alithibitisha pia beki Gabriel Paulista amesafiri na timu kwenda Monaco baada ya kupona kutokana na tatizo la misuli.
Mechi hii ina maana kubwa kwa Wenger pia: ambaye alikuwa meneja katika klabu ya Monaco kwa miaka saba, na kuiongoza kutwaa kombe la Ligi ya Ufaransa mwaka wa 1988 na pia kombe la Ufaransa , kabla ya kuhamia Japan na kisha katika klabu ya Arsenal mwaka 1996.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments