Ticker

6/recent/ticker-posts

BAADA YA MIEZI CHINI YA 18 TU,GUS PUYET WA SUNDERLAND AMEKUTWA NA JAMBO

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.March.17,2015 SAA 09:20 USIKU
Gus Poyet: Replaced Paolo Di Canio at Sunderland

Sunderland imemfukuza kazi meneja wake Gus Poyet baada ya kushinda mechi moja tu kati ya 12 zilizopita za Ligi Kuu ya
England.

Meneja huyo wa Paka hao Weusi amedumu kwa miezi 17  katika klabu hiyo inayoning'inia katika nafasi ya 17 baada ya kufungwa mabao 4-0 na Aston Villa siku ya Jumamosi.

Poyet amekutana na mkurugenzi mkuu Margaret Brrne pamoja na wajumbe wengine wa bodi baada ya mazoezi siku ya Jumatatu,na kuambiwa kuwa muda wake ulikuwa hadi baada ya miezi chini ya 18.

  
Poyet raia wa Uruguay, ambaye aliiokoa klabu hiyo kutoka kushuka daraja, alichukua umeneja wa Sunderland mwezi Oktoba 2013, kuziba nafasi ya Paolo di Canio.

Aliingoza timu hiyo katika mechi 75, akashinda mechi 23, akapoteza 22 na sare 30.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments