Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh. milioni tatu kutokana na timu yake kuvaa jezi
ambazo hazikuwa na nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.
Mechi hiyo namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom ilichezwa Desemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 13(7) ya Ligi Kuu inayotaka klabu kuheshimu masharti ya udhamini wa Ligi Kuu kwenye mechi zake.
Wachezaji wa Simba na JKT Ruvu wakisalimiana Jana kabla ya mchezo uliomalizika kwa Simba Kushinda kwa mabao 2 kwa 1 |
Kikosi cha Simba |
Kikosi cha JKT Ruvu |
Nayo Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 28(4) kwa kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na Toto Africans iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuvurugika.
Kutokana na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 28(1) inayotawala ligi hiyo.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments