Ticker

6/recent/ticker-posts

VIDEO:RIO FERDINAND NA KOCHA WAKE WAWABWATUKIA MASHABIKI WA CHELSEA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Feb.19,2015 SAA11:36 JI0NI

Mchezaji wa Queens Park Rangers  Rio Ferdinand na Chris Ramsey wamekuwa watu maarufu wa mwanzoni kuonyesha
hisia kali baada ya mashabiki wa Chelsea kumzuia mtu mweusi kuingia katika behewa la treni mjini Paris.

Nahodha huyo wa zamani wa England Ferdinand anaamini soka limefanya mengi ya kupambana na ubaguzi wa rangi na kwamba tatizo pana lipo katika jamii kwa ujumla, lakini alihoji kama mamlaka husika zinafanya jitihada za kutosha kukabiliana na tatizo?.

Mashabiki hao wa Chelsea wengine walikuwa wakiimba nyimbo za kibaguzi - wakati wa mechi ya siku ya Jumanne ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Paris Saint-Germain.

Katika mfululizo wa ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, Ferdinand alisema ubaguzi na tabia mbovu ya baadhi ya mashabiki wa Chelsea-ilidhihilika wazi,na kuuliza kuwa soka linaweza kubadilisha hili? na kuongeza kuwa  watu katika mchezo kwamba wanatakiwa kuwekeza  nguvu kweli katika kutokomeza ubaguzi wa rangi.
QPR manager Chris Ramsey
Wakati huo huo Ramsey ambaye ni bosi na kocha mkuu Ferdinand wa sasa katika dimba la Loftus Road, pia amekemea swala hilo lililofanya katika mji mkuu wa Ufaransa.
Ramsey, ambaye ni meneja mweusi pekee katika Ligi Kuu, alizungumza wakati wa maswali kuhusu hilo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari juu ya  mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Hull.

"Siamini kwamba wao ni mashabiki wa Chelsea," alisema. "Siamini kwamba wao ni mashabiki wa soka. Wametugusa na sisi sote kwa namna moja,nafikiri ni jambo la zamani. Napenda kuwalaumu Chelsea Football Club kwa hilo.”alisisitiza  Chris Ramsey

ANGALIA VIDEO YA TUKIO LA KIBAGUZI LILILOFANYA NA MASHABIKI WANAOAMINIKA NI WA CHELSEA


 KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments