Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:MATOKEO YA LIGI TZ BARA,SIMBA YAIANGAMIZA TZ PRISONS 5 -0,JAMHULI KIHWELO "JULIO" AANZA VYEMA NA COASTAL UNION,STAND UNITED YABAKISHA KIPORO KESHO,MBEYA CITY NA RUVU SHOOTING JE ?

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Feb.28,2015 SAA 03:03 USIKU

Ibrahim Ajib amefanikiwa kuwapa raha mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi Simba hii leo, baada ya Kupiga mabao Matatu peke
yake (Hat-Trick) katika ushindi mzito wa klabu hiyo wa Mabao 5 - 0 dhidi ya Timu ya Tanzania Prisons, mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Tanzania Prisons

Kikosi cha Simba



(Kutoka Kushoto) Kocha wa Simba Goran Kopunovic,wa pili ni Suleman Matola
(Kulia)Kocha wa Tanzania Prisons David Mwamaja




Mabao matatu ya Ibrahim Ajib yalipatikana katika kipindi cha kwanza,katika dakika ya 15 Ibrahim Ajib aliipatia bao la kwanza Simba baada ya kupokea pasi kutoka kwa Dan SSerenkuma aliyeukokota mpira baada ya kuzongwa na Mabeki wa Tz Prison na kumpasia Ajib aliyeweka mpira nyavini.

Goli la pili Ibrahim Ajib alifunga dakika 21 alitumia Vizuri makosa ya mlinda lango wa Tz Prison Mohamed Yussuf baada ya kulitema shuti la mshambuliaji Emmanuel Okwi.



Mchezaji wa Tz Prison Lugano Mwangama aliunawa mpira katika Eneo la hatari,na Ibrahim Ajib akakamilisha Hat-Trick yake dakika ya 41 kwa kupiga mkwaju wa penalti.




Mabao mawili ya Simba yalipatikana kipindi cha pili,ambapo Emmanuel Okwi dakika 75 alifunga bao la 4 na kisha kutengeneza pasi iliyozaa bao la 5 alilofunga Ramadhan Singano "Messi" dakika ya 84 na mchezo kumalizika kwa Simba kuichapa Tz Prisons mabao 5 - 0 .


Shabiki wa Simba alizimia Uwanjani

Akipelekwa Hospitali


MATOKEO YA MICHEZO MINGINE

Katika Dimba la Kambarage Mchezo kati ya  Stand United na Kagera Sugar ulivunjika katika dakika ya *80' ,na wakati huo timu ya Stand United ilikuwa ikiongoza kwa 1 - 0 dhidi ya Kagera Sugar, mechi haikumalizika kutokana na kunyesha mvua kubwa,na  mchezo huo utamaliziwa kesho kwa kuchezwa dakika 10 zilizobakia.

FT' Mgambo Shooting 0 - 1 Coastal Union-  Mkwakwani

FT' Mbeya City 1 - 1 Ruvu Shooting-
 Sokoine


 KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .


Post a Comment

0 Comments