Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea hii leo kwa michezo mitatu iliyopigwa katika viwanja tofauti Tanzania Bara.
Ndanda Fc ilikuwa ikiwaalika Mtimbwa Sugar katika uwanja wa Nangwanda Sijaona,mchezo ambao ulimalizika kwa Sare ya bila kufungana 0- 0.
Mchezo uliopigwa katika Dimba Kambarage mkoani Shinyanga,ulishuhudiwa Timu ya Stand United ikichomoka na ushindi mnono wa mabao manne kwa moja 4- 1 dhidi ya timu ya Mgambo Jkt.
Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya timu ya Coastal Union na Mbeya City,mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,na matokeo ya mwisho ya mchezo huo ni kwamba umemalizika kwa sare ya bila kufungana 0 - 0.
MECHI ZA KESHO Feb 15-
MECHI ZA KESHO Feb 15-
Polisi Morogoro vs Simba
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

0 Comments