TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga imeitumia salama
timu ya Yanga kuwa isitarajie itaweza kuchukua pointi tatu kirahisi kwenye
mechi yao itakayochezwa Jumatano wiki hii ya Ligi kuu kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani badala yake ijiande kwa kipigo kutokana na maandalizi walioyafanya kuelekea mchezo huo.
mechi yao itakayochezwa Jumatano wiki hii ya Ligi kuu kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani badala yake ijiande kwa kipigo kutokana na maandalizi walioyafanya kuelekea mchezo huo.
Akizungumza LEO,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa asilimia kubwa ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye
timu hiyo yamefanyiwa marekebisho na kikosi cha timu hiyo kipo tayari kuweza
kuwakabili wana jangwani hao kwa kupata ushindi.
Amesema kuwa katika mechi zake alizocheza
amekijua vema kikosi hicho hivyo anaamini dozi ambaye ameanza kutoa kwao
itaweza kuwabadilisha vilivyo kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye michezo
yao ya ligi kuu soka Tanzania bara.
“Tokea
tulipomaliza mechi yetu na JKT Ruvu tumekuwa tukiwapa wachezaji wetu mazoezi ya
nguvu kuhakikisha safu mbalimbali zinaimarika kabla ya kuwavaa Yanga, ninaamini
tutafanya vema kwa sababu timu zote za Ligi kuu soka Tanzania bara zitahitaji
pointi tatu nasi tunahitaji hizo hizo “Amesema Assenga
Akizungumzia hali za wachezaji, Kocha Mkuu wa timu hiyo,James Nandwa amesema
wachezaji wote wapo imara kwa ajili ya mchezo huo ambao kwa lengo la
kuhakikisha wanapambana vilivyo ili kuweza kubakiza pointi tatu kwenye uwanja
wao wa nyumbani mkwakwani.
Coastal Union itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa ni
kumbukumbu ya kupoteza mechi yao na Jkt Ruvu kwa kufungwa bao 1-0 kwenye uwanja
wake wa nyumbani
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments