Anthony Hamilton: anadhani Lewis Hamilton anaweza kushinda taji jingine katikati ya 2015 |
Anthony Hamilton amemtabiria mwanawe Lewis Hamilton kuwa anaweza kushinda taji la F1 la 2015 pamoja na la
katikati ya msimu.
Dereva huyo wa Mercedes alipata taji lake la pili la michuano ya dunia katika mashindano ya mwisho wa msimu 2014 huko Abu Dhabi baada ya mwaka-mrefu wa mapambano na mchezaji mwenzake Nico Rosberg.
Hata hivyo baba huyo wa Lewis Hamilton anadhani bila matatizo yoyote ushindi wa taji unaweza kupatikana hata mapema.
"Huwezi kujua, lakini nadhani kama ukiangalia nini alichokifanya Lewis mwaka jana, sisi tumeanza mwaka ambapo tunaona kwamba kila kitu kinakwenda vizuri, na katikati ya mwaka yeye pengine angalishinda michuano," aliiambia Sky Sports Online.
"Nadhani kitu kinaweza kuwezekana na kutokea mwaka huu -. Kama amenza vizuri, kama gari ni nzuri, utendaji ni mzuri, nadhani Lewis anaweza kushinda ubingwa tena mwaka huu"
Hata hivyo, Anthony Hamilton anajua itakuwa si rahisi kwa mwanawe, kwani Rosberg alionesha kiwango kizuri waliposhindana 2014.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments