Ticker

6/recent/ticker-posts

GARETH BALE AFURAHIA USHINDI WA WALES

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.OCT.12,2014 SAA 04:52  USIKU 

Gareth Bale anasema kikosi cha Wales kiko katika hali ya matumaini baada ya kuwafunga Cyprus na kubakia katika
mstari kwa ajili ya kufuzu michuano ya Euro 2016.

Ushindi wa 2-1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Cardiff City usiku wa Jumatatu, umewafanya vijana Chris Coleman kuongoza Kundi B, wakiwa na pointi saba kutokana na michezo yao mitatu ya Ratiba ya ufunguzi.

Kikosi cha Wales kilikuwa katika hali ngumu baada ya mchezaji wao, Andy King kutolewa nje mapema katika kipindi cha pili na kutishia kikosi hiko kilichoanza vizuri.

Wales walikuwa na uwezo wa kufanya vizuri zaidi, ingawa, Bale ambaye ni mchezaji wa ghali zaidi katika ulimwengu wa kandanda - aliongoza kama mfano katika mchezo huo.

Bale aliiambia Sky Sports: "tulianza kucheza kwa nguvu tena"
"tulikuwa nje ya kile tulichokifikiri,tulianza vizuri katika mchezo. Ni wazi kuna makosa madogomadogo , lakini unaweza kuona ni kiasi gani vijana hawa wanachokiitaji".
"tuna hisia tofauti katika kambi ya sasa, kila mmoja kwa kweli anapigana kwa ajili ya kila mmoja, timu imehamasika na mashabiki, tena wamekuwa na hamasa kubwa.
"Unahitaji kidogo bahati wakati mwingine. Nadhani tumeonyesha kufanya kazi kwa bidii tangu tufanye makosa, tunafanya kazi kwa bidii kama timu"

Mabao ya Wales yalifungwa na David Cotterill pamoja na Hal Robson-Kanu katika kipidi cha kwanza,huku bao la kufutia machozi la Cyprus akifunga Vincent Laban.


Mchezo unaofuata Wales watafunga safari mpaka Ubelgiji tarehe 16 Novemba, kwa ajili ya mtihani mwingine, lakini Bale anasema vijana wa  Coleman hawana hofu na wana ujasiri kuwa wanaweza kupata matokeo mazuri.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments