Timu ya Brazil katika usiku wa kuamkia Jana iliichapa bao 1 kwa 0 timu ya Colombia katika mchezo uliokuwa wa kirafiki
wa kimataifa.
wa kimataifa.
Bao pekee katika dakika ya 83 liliiwezesha Brazil kuondoka na ushindi huo mwembamba kwa bao la mkwaju wa Free Kick la Naymar.
Colombia walikuwa pungufu baada ya Juan Cuadrado kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Naymar Dk.50 ya mchezo huo ambao Brazil ilikuwa ikiongozwa na kocha wa mpya Dunga.
Katika mchezo huo pia Naymar ambaye alikuwa Nahodha wa Brazili,alionyesha kitendo cha kiungwana kwa kupeana mkono kwa furaha pamoja na kukumbatiana na Juan Zúñiga ambaye naye alikuwa Nahodha,ambapo mchezaji huyo ndiye aliyemsababishia majereha ya mgongo katika kombe la dunia nchini Brazil.
ANGALIA PICHA, NA CHINI KABISA KUNA VIDEO
Mechi ya ushindi:Nyota wa BarcelonaNeymar alifunga bao pekee la mchezo huo dakika ya 83 |
Zuniga alimlazimisha Neymar kukosa mechi kadhaa za Kombe la Dunia 2014 |
Neymar alitolewa nje kwa kubebwa kwenye machela wakati wa ushindi mwembamba wa Brazil katika Kombe la Dunia dhidi ya Colombia
|
VIDEO
0 Comments