Simba Sc imetuma salamu kwa timu zinazishiriki ligi kuu msimu wa 2014- 2015 baada ya ya hii leo kuwaonesha balaa timu ya Gor
Mahia ya Kenya kwa kuitandika mabao 3 kwan 0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mahia ya Kenya kwa kuitandika mabao 3 kwan 0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Emmanuel Okwi akiingia uwanjani na wachezaji wenzake |
Kikosi kilichoanza |
Benchi la Gor Mahia |
(Kushoto) ni kocha mkuu wa simba Patrick Phiri |
Simba ambao walimchezesha mchezaji wao Emmanuel Okwi ambaye amerejea katika kikosi hiko baada ya kuitumikia Yanga katika msimu uliopita,mabao yalifungwa na washambuliaji wawili Paul Kiongera na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba Advocate,Dkt.Damas Daniel Ndumbaro,akisalimiana na Kocha Mkuu wa Young Africans Marcio Maximo kabla ya mechi. |
Emanuel Okwi alikuwa katika wakati mgumu kwani kila akigusa mpira mashabiki wanaosemekana ni wa Yanga walikuwa wakimzomea |
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu hizo kwenda mapumzika bila kufungana,lakini kutokana na maelekezo ya kocha Patrick Phiri vijana hao wa msimbazi walirudi na kasi ya ajabu katika kipindi cha pili.
Kocha Mkuu wa Young Africans Marcio Maximo akisalimiana na mashabiki |
Mabao mawili ya Simba yalifungwa na Paul Kiongera dakika ya 51 na 77 huku Ramadhani Singano ‘Messi’alifunga bao la pili katika dakika ya 66.
Uhuru sulemani |
Ramadhani Singano ‘Messi’ na wachezaji wenzake wa Simba wakishangilia bao la pili |
Paul Kiongera akifunga bao la tatu kwa Simba katika mchezo huo |
Paul Kiongera na Ramadhani Singano ‘Messi’wakishangilia bao la Tatu kwa timu ya simba |
(Kushoto )Kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola akiwa na kocha mkuu wa simba Patrick Phiri |
0 Comments