Beki wa Manchester United Marcos Rojo sasa yuko huru kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya QPR baada ya
kupokea kibali cha kufanya kazi.
" Shirika la Uingereza limekubali kutoa visa kwa beki wa #mufc MarcosRojo5 na kwa hiyo atapatikana katika mechi dhidi ya QPR tarehe 14 Septemba," ilisema taarifa hiyo rasmi ya United kwenda kwa vyombo vya habari.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amesaini katika klabu hiyo kutoka Sporting Lisbon kwa ada ya £ 16m mwezi uliopita, lakini imekuwa hapatikani katika michezo kwa sababu ya kutopata kibali cha kumuwezesha kufanya kazi nchinin UK – kitu kinachomfanya timu yake ishindwe kupata idhini ya premier league kumchezesha mchezaji huyo.
0 Comments