Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Sept.17,2014 SAA 01:16 USIKU
Maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Jumamosi hii septemba 20 yako katika hatua nzuri kwa maana ya
Viwanja,ambapo bodi ya Ligi Iko katika Ukaguzi wa mwishoni wa Viwanja.
Lakini kwa upande wa vilabu wanaitazamaje ligi hiyo?
Leo tuanza na Mabingwa watetezi Azam Fc,Ambapo Jamii na michezo imezungumza na kocha msaidizi wa wa timu hiyo Kali Ongala Ambapo kocha huyo amesema wao kama mabingwa watetezi bado wanazidi kujipanga kutetea ubingwa wao,lakini anaamini ligi ya mwaka huu itakuwa ngumu zaidi.
"Kama ninavyosema kila siku mwaka huu Ligi itakuwa ngumu zaidi,sisi ndio mabingwa watetezi na kila mtu anataka kumfunga bingwa,kwaio tunajua haitakuwa na kazi raisi,mabingwa watetezi tunataka kutetea ubingwa wetu,tutajipanga vizuri zaidi"alifafanua Ongala
Aidha Ongala akaongelea mchezo wa Ngao ya Jamii ambao walipoteza dhidi ya Yanga kwa kufungwa mabao matatu kwa sifuri,"nadhani mechi hii sio kama tumeidhalau lakini tulikuwa na hofu sana,muda mwingine unajua kuna mchanganyiko wa vitu vingi,sisi tumetoka Rwanda,tulifikili tumejiweka levo frani lakini uzuri tumekutana na hali halisi,lakini muhimu zaidi tulikuwa tunataka kushinda lakini tumefungwa na tumejifunza kitu frani kwa kufungwa"alisema Kali Ongala.
Pia Ongala hakusita kuomba msamaha kwa mashabiki kutokana na mchezo huo."Samahani kwa Washabiki wote wa Azam Fc,tumecheza chini ya kiwango,tuko vizuri na tunajua sisi ni zaidi ya hilo,kwa hiyo tunaomba watusamee,kwani ni bora tumefungwa leo kuliko kesho"alimazia Kali Ongala.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments