Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.JUL.12,2014 SAA 02:40 USIKU
Kiungo wa Arsenal Mikel Arteta imekataa taarifa juu yake kuwa kunauwezekano wa kuondoka katika klabu yake
msimu huu.
Ripoti za hivi karibuni zimedai kuwa timu kutoka Italia, Fiorentina walikuwa na shauku ya kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa Everton.
Wakala wa Arteta alikataa uvumi huo na kusisitiza Mhispania huyo amekuwa na furaha na maisha yake akiwa Arsenal.
"Siwezi kusimamisha uvumi, lakini hakika ni kwamba Najisikia furaha sana hapa,nahisi thamani," alisema Arteta.
Arteta pia alisifia usajili wa Alexis Sanchez kutoka Barcelona akionyesha hisia zake na ishara halisi ya kufanya vizuri kwa Arsenal kabla ya msimu mpya
" ni aina ya mchezaji tuliyekuwa tunamtafuta," aliongeza Arteta.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments