Ticker

6/recent/ticker-posts

NANI KUSHINDA KIATU CHA DHAHABU KOMBE LA DUNIA? FIFA YATANGAZA WACHEZAJI 10 WANAOWANIA TUZO HIYO

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.JUL.11,2014 SAA 04:29 USIKU
Wajerumani wanne ni miongoni mwa wachezaji 10 waliochaguliwa kwa ajili ya kuwania kinyang'anyiro tuzo ya
kiatu cha Dhahabu katika mashindano ya Kombe la Dunia kama mchezaji bora.

Mats Hummels, Toni Kroos, Thomas Muller na Nahodha Philipp Lahm wote wako katika mbio hizo za kifahari na heshima zilizoandaliwa na FIFA .

Mchezaji anayefuatiliwa kwa sasa kutoka Colombia  James Rodriguez, ambaye alifunga mara sita kabla ya nchi yake kuondolewa katika robo fainali naye pia ameteulewa kuwania tuzo hiyo.

Neymar Mchezaji pekee kutoka Brazil ambaye ameteuliwa, na Winga wa Uholanzi Arjen Robben pia akiwepo katika kinyang'anyiro hicho.

Wa Argentina watatu wanakamilisha orodha hiyo- Lionel Messi, Angel Di Maria na Javier Mascherano.

Tuzo hiyo - alishinda mchezaji wa Urugwai  Diego Forlan miaka minne iliyopita - ni kura iliyokuwa na mchanganyiko wa kamati ya FIFA ya kiufundi na wawakilishi wa vyombo vya habari.

FIFA pia ilitangaza kuwateua makipa watatu wanaowania tuzo ya Glove za Dhahabu  kwa kipa bora: nao ni kutoka Ujerumani Manuel Neuer, Sergio Romero wa Argentina na Keylor Navas wa Costa Rica.

Na pia kuna wale naowania tuzo ya mchezaji anayechipukia katika mashindano: nao ni Memphis Depay wa Uholanzi na kutoka Ufaransa ni Paul Pogba pamoja na Raphael Varane.

Washindi watatangazwa baada ya mchezo wa fainali siku ya Jumapili.

TOA MAONI YAKO, NANI KUSHINDA TUZO YA KIATU CHA DHAHABU KATIKA KOMBE LA DUNIA ?

  •  Angel Di Maria
  •  Mats Hummels
  •  Toni Kroos
  •  Phillip Lahm
  •  Javier Mascherano
  •  Lionel Messi
  •  Thomas Muller
  •  Neymar
  •  Arjen Robben
  •  James Rodriguez

    ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA      (Jamii na Michezo) 

    TOA MAONI YAKO

Post a Comment

0 Comments