Mshambuliji wa Italia Mario Balotelli huenda akafikishwa mahakamani kufuatia kuleta utata baada ya kuchapisha
picha yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa ameshika bunduki na kuielekeza katika kamera na kuambatanisha na ujumbe usemao "kiss kubwa kwa maadui wote".
Mchezaji huyo wa AC Milan aliondoa haraka picha hiyo, lakini matukio ya hivi karibuni huenda yakamfanya aonekane anataka kuleta madhara nchini Italia ambapo yeye imekuwa akinyanyaswa mara kwa mara kwa ubaguzi wa rangi, na amekuwa na hali ngumu ya kukatishwa tamaa katika kampeni za Kombe la Dunia nchini Brazil.
0 Comments