Argentina wamepigwa faini ya $336 000 kwa kushindwa kupeleka wachezaji katika mkutano na waandishi
wa habari kabla ya mechi wakati wa Kombe la Dunia, FIFA wamesema katika taarifa yake siku ya Ijumaa.
Kamati ya Fifa ya kinidhamu alisema Argentina alikuwa imevunja kanuni ya vyombo vya habari katika mikutano wa habari kwa siku hiyo kabla ya mchezo dhidi ya Nigeria, Uswisi, Ubelgiji na Uholanzi,huku kocha Alejandro Sabella tu akiuzulia .
kocha anatakiwa kuonekana pamoja na mchezaji.
"Lengo .. ni kuruhusu vyombo vya habari, na hatimaye mashabiki kupata nafasi ya kufuatilia maandalizi ya timu, pia kuruhusu kila timu kuwa na mazingira bora kwa ajili ya maandalizi," kiongozi wa FIFA alisema.
Hakuna majibu ya haraka kutoka kwa Argentina, ambao watakabiliana na Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia siku ya Jumapili.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments