Kamati ya FIFA ya kinidhamu haitachukua hatua yoyote dhidi ya mchezaji wa Colombia Juan Zuniga kwa ajili ya
changamoto ambayo ilisababisha kuumia kwa Nyota wa Brazil Neymar.
Mfupa wa Neymar unaoshikana na uti wa mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia,ambapo Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.
Mwamuzi wa Uhispania Carlos Velasco Carballo hakumwonesha Zuniga kadi ya njano na Shirikisho la soka la Brazil lililalamika kwa FIFA kuhusu hali hiyo -na kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari alidai Mcolombia huyo alikuwa "Anamuwinda" Neymar.
Jopo la Kinidhamu la FIFA , ambalo lilikuwa chini ya mwenyekiti Claudio Sulser, waliangalia video ya tukio hilo lakini waliamua jambo hilo chini ya sheria kama tukio la bahati mbaya lililonekana na viongozi wa mechi.
hawakutaka kufungua kesi dhidi ya Zuniga, ambaye alimuomba radhi kwa Neymar siku ya Jumamosi.
Taarifa ya FIFA inasema: "mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya FIFA anasikitika kwa tukio hilo lililokuwa na madhara makubwa kwa afya Neymar ".
"Hakuna hatua inayoweza kuchukuliwa ukilinganisha na matukio ya nyuma ya mchezaji huyo wa Colombia Juan Camilo Zuniga Mosquera kwani hakuwai kuwadanganya maafisa makini wa mechi"
"Hali ambayo kamati ya FIFA ya nidhamu inaweza kuangilia katika tukio lolote na kuchukuliwa matokeo ambayo yatategemewa na tukio hilo, kama amejeruhiwa kwa bahati mbaya au la"
"Tunamtakia Neymar auheni haraka na tunataka awe sawa kama wachezaji wote ambao wako katika masikitiko kutokana na kukosa Kombe la Dunia kwa sababu ya kuumia."
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments