Kocha wa Nigeria ambao ni Mabingwa wa Afrika 2013,Stephen Keshi amejiuzulu wadhfa wake katika timu
hiyo .
hiyo .
Keshi amejiuzulu punde baada ya timu ya Super Eagles kuondolewa kutoka kwenye kipute cha kombe la dunia ilipolazwa 2-0 na Ufaransa .
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alichukuwa wadhfa huo mwaka wa 2011 na Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Keshi kujiuzulu wadhfa wakae,itakumbukwa mwaka wa 2013 Keshi alikuwaradhi kujiuzulu lakini akashawishiwa kusalia kama kocha na waziri wa michezo wa Nigeria.
Chini ya uongozi wake Super Eagles imefuzu kwa mara ya kwanza katika mkondo wa pili wa kombe la dunia tangu mwaka wa 1998 licha ya kukumbwa na migomo ya mara kwa mara ya wachezaji wake wakidai malimbikizi ya marupurupu yao.
Kuondoka kwake kumefikisha idadi ya wakufunzi waliojiuzulu kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia kutimia makocha 6.
Makocha wengine waliondoka ni pamoja na Luis Fernando Suarez, wa Honduras, Carlos Queiroz wa Iran's , Alberto Zaccheroni wa Japan , Cesare Prandelli wa italia na Sabri Lamouchi wa Ivory Coast.
Keshi, aliwahi kuwa kocha wa Mali pamoja na Togo.
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
CHANZO:BBC
0 Comments