Uvumi uliozuka wiki iliyopita kuwa kocha Alejandro Sabella amepoteza ushirikiano kwa wachezaji wa Argentina ndani ya
vumba vya kubadilishia nguo ,umezua jambo baada ya mshambuliaji Ezequiel Lavezzi kuonekana akimwagia maji kocha huyo wakati wa mchezo ambao timu ya Argentina ilipoifunga Nigeria mabao 3 kwa 2.
Kwa mujibu wa ripoti wa timu ya Argentina alisema katika kipindi cha pili wakati wa mechi ya ufunguzi walioibuka na ushindi dhidi ya Bosnia-Herzegovina, inadaiwa kuwa Sabella alibadili mfumo kutoka 5-3-2 na kuwa 4-3-3 ambao nahodha Lionel Messi aliupendelea.
Maji yaliyokuwa katika chupa yalimrukia kwa bahati mbaya kocha Sebella wakati Lavezzi alipokuwa anakunya huku akipewa maelekezo katika kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya Nigeria, na kuacha maswali kwa mashabiki wengi kuwa labda mchezaji huyo alifanya makusudi,wakilinganisha na taarifa za awali za kocha huyo kutokuwa na maelewano na wachezaji wake.
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
ANGALIA VIDEO YA TUKIO
0 Comments