Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.Jun. 07,2014 SAA 11:46 JIONI
Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi, Anatarajiwa kuchukua uamuzi wa mwisho
juu ya beki wa kushoto wa AS Monaco, Elderson Echiejile, mwishoni mwa wiki hii,katika kampeni kuelekea fainali za Fifa za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Echiejile imekuwa nje tangu apatwe na maumivu ya msuli katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Ugiriki na imekuwa akipewa mafunzo tofauti na kikosi,chini ya usimamizi wa daktari wa timu, Ibrahim Gyaran.
Mlinzi huyo wa zamani wa Sporting Braga, amekwisha kufanyiwa uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo bado hayajawekwa wazi.
"Bado Hakuna matokeo ya mwisho kwa mchezaji Elderson. Daktari wa timu amekuwa akifanya kazi juu yake ,na uamuzi wa mwisho utafanywa baadaye, juu ya hali yake na kocha mkuu (Stephen Keshi)," msemaji wa mabingwa hao wa Afrika, Ben Alaiya, aliiambia Supersport . com moja kwa moja kutoka mjini Jacksonville huko USA siku ya leo Jumamosi.
Keshi pia aliunga mkono maneno hayo wiki hii kwamba hakutakuwa na uamuzi haraka juu ya mchezaji huyo,na yeye anatarajiwa kumchukuwa mchezaji mwingine katika kikosi cha Nigeria kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Echiejile pia hatakuwepo katika mchezo wa kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya fainali za Kombe la Dunia katika mechi ambayo itapigwa baadaye hii leo Jumamosi na timu ya USA
Nigeria bado wanaruhusiwa kufanya mabadiliko kwa kesi ya Echiejile, kama mchezaji huyo atawekwa kando kwa ajili ya Kombe la Dunia kabla ya mchezo wao wa kwanza dhidi ya Iran siku ya Juni 16.
.
0 Comments