Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.Jun. 05,2014 SAA 10:33 JIONI
Kuanzia tarehe 14 mwezi Juni,2014 Tamasha nchi za Majahazi litakuwa linasherehekea miaka 17 ya tamasha hilo toka
lianzaishwe.ZANZIBAR INTERNATION FILM FESTIVAL kwa kifupi (ZIFF) imefanya uzinduzi wa tamasha rasmi wa tamasha hilo kwa kufanya mkutano na vyombo vya habari siku ya leo Alhamisi tarehe 5 katika ukumbi wa GOETHE INSTITUTE Dar es salaam.
|
Mkurugenzi mkuu wa ZIFF Prof.Martin Mhando akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) |
"Takribani filamu 79 zitaonyeshwa kwa siku 10 katika tamasha la mwaka huu kutoka katika nchi kadhaa za Afrika na nchi za majahazi zikiongozwa na filamu kadhaa ambazo zimeshawahi kushiriki kushinda tuzo katika matamasha mbalimbali duniani,Filamu za mwaka huu zinatoka katika nchi 35 ambapo 38 ni filamu fupi,23 filamu ndefu na 18 zitakuwa filamu za makala" alisema mkurugenzi mkuu wa ZIFF Prof.Martin Mhando.
|
Mmoja wa wasanii watakaoshiriki akizumgumza |
|
Muwakilishi wa Fastjet akizungumza |
|
Msanii wa Hip Hop one incredible atashiriki katika tamasha hilo |
|
Mwanamuziki Mzungu Kichaa pia atashiriki katika tamasha hilo |
Fastjet ambao ni shirika la usafili wa angani limedhamini Tamasha hilo kwa mara ya kwanza.Ratiba rasmi ya filamu itaoneshwa pamoja na taarifa kuhusu majukwaa ya wanawake na vijijini,mwaka huu takribani wanafunzi 2000 watapata nafasi ya kuangalia filamu za watoto na kuzijadili katika jukwaa la watoto ikiwa ni sehemu ya udhamini wa shirika la Save the Children Zanzibar.mada kuu ya mwaka huu itahusu Mazingira na kauli mbiu itakuwa "MAZINGIRA SALAMA"
|
Mmoja wa Ma DJ atakayeshiriki katika tamasha hilo |
|
Wadau mbalimbali wakisikiliza |
Pia ZIFF itawasilisha taarifa kuhusu jukwaa la muziki na wasanii watakaoshiriki katika tamasha pamoja na maonesho ya kazi za mikono (exhibitions) na baraza la wataarishaji filamu.Wadhamini wakuu wa ZIFF kwa miaka 10 Zuku watapata nafasi ya kuzungumza kuhusu kujikita kwao katika kudhamini tamasha hili.Richard Alden ambae ni mkurugenzi mkuu wa ZUKU alisema "Tamasha hili ni alama ya historia ya Zanzibar katika filamu na pia kuonesha jitihada kubwa ya tamasha hili katika kuunganisha pamoja watengenezaji wa filamu wenyewe wa kisiwa hichi ambapo hakuna majumba ya kuoneshea filamu toka yalipofunguliwa mwaka 1990.
Katika hatua nyingine mkurugenzi mkuu wa ZIFF Prof.Martin Mhando amesema bado wanafanya jitihada za kuweza kumleta Lupita Nyong'o,lakini wanauhakika kuwa familia yake yaani Mama,Baba na Dada wa Lupita Nyong'o, watakuwepo katika muda wote wa siku 10 za tamasha hilo.
Lupita Nyong'o pia ameanzia ZIFF maswala yake ya FILM katika miaka ya 2006 na 2007.
0 Comments