Gerardo 'Tata' Martino ameacha kazi kama meneja wa FC Barcelona baada ya mechi dhidi ya Atletico Madrid.Raia
huyo wa Argentina, ambaye alifuatana na Andoni Zubizarreta, alitangaza uamuzi huo baada ya mechi katika mkutano na vyombo vya habari "Natangaza maaamuzi yangu pamoja na Club ya kusimama kusimamia klabu ya FC Barcelona," alisema. Aliendelea kwa kushukuru, "bila kujali matokeo ya leo,"

"Nashukuru Club kwa kila kitu kutoka kwangu, na mshukuru Rais Bartomeu Mkurugenzi Zubizarreta na Sandro Rosell kwa kuwa na imani na mimi." Aliongeza: "Nawashukuru pia mashabiki kwa heshima yao, na namshukuru kila mtu kwa kufanya kazi pamoja nami na wafanyakazi wenzangu, na hasa nawashukuru wachezaji. "
Katika hatua nyingine hii leo Lionel Messi amesaini rasmi mkataba bora na klabu hiyo mbele ya Rais Josep Maria Bartomeu pamoja na baba yake ambaye ni meneja wake.
Maelezo ya mkataba mpya wa messi hayako wazi, lakini mkataba huo umefuatia majadiliano ya muda mrefu.
Lionel Messi imekubali mkataba huo mpya na klabu ya Barcelona ambao utafanya kuwa mchezaji anayelipwa kiwango kikubwa kuliko wachezaji wote.
Imeripotiwa kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 26 alisisitiza juu ya kumpita mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo katika kiwango cha kulipwa kama mchezaji bora duniani.
0 Comments