Ticker

6/recent/ticker-posts

LUIS ENRIQUE MENEJA MPYA WA FC BARCELONA ASAINI MKATABA WA MIAKA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 19,2014 SAA 5:00 USIKU
Luis Enrique seated and smiling

Bodi ya Wakurugenzi ya FC Barcelon imethibitisha kuwa Luis Enrique Martíneza ni kocha mpya wa timu ya kikosi cha
kwanza, na hiyo ni kutokana na pendekezo la Mkurugenzi wa Michezo Andoni Zubizarreta. Luis Enrique, 44, amesaini mkataba wa miaka miwili.

 Luis Enriqu anarudi katika klabu hiyo kwa mara nyingine, baada ya awali alipojiunga kama mchezaji akitokea Real Madrid mwaka 1996 hadi 2004.


Katika misimu yake mitatu ya kwanza alishinda makombe ya Ligi mara mbili, ​vikombe viwili vya hispania , kombe la mabingwa na European Super Cup. Katika miaka yake minane kama mchezaji, Luis Enrique alicheza michezo 300 na kufunga mabao 109 na alikuwa nahodha 2002-2004, na mwishoni akanyakua kiatu cha zahabu kama mchezaji bora .

Alivunja rekodi kama kocha na timu B

Mwaka 2008, alilirudi katika klabu ya Barca, kuchukua nafasi kama kocha wa kikosi B cha Barca na baada tu ya kukosa katika mwaka wake wa kwanza, aliivusha timu yake katika ligi daraja la pili kwa mara ya pili, kwa kuwaongoza vijana hao kuvunja rekodi ya pointi na kumaliza msimu wa 2010/11 katika nafasi ya tatu.
.@LUISENRIQUE21 te deseamos lo mejor posible como nuevo entrenador del @FCBarcelona_es: adelante Luis!


Post a Comment

0 Comments