Ticker

6/recent/ticker-posts

UCHAGUZI SIMBA:MAMBO YAZIDI KUPAMBA MOTO,MCHAKATO WAFIKIA HATUA YA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 19,2014 SAA 9:00 USIKU
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba Advocate,Dkt.Damas Daniel Ndumbaro,akizungumza
Kamati ya Uchaguzi wa Simba hii leo imeanza kupokea pingamizi kwa wagombea wote 41 wa klabu hiyo, waliopitishwa baada ya
kutimiza masharti yaliyowekwa katika fomu za uchaguzi wa klabu ya Simba Sports Clabu.

Mapingamizi hayo ambayo yanapokelewa na naibu katibu wa kamati ya uchaguzi katika ofisi za klabu hiyo,yatafikia tamati kupokelewa siku ya  kesho  kutwa tarehe 22.

Kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Advocate,Dkt.Damas Daniel Ndumbaro,inakumbusha Pingamizi zote ziwasilishwe kwa maandishi ikiambatana na Vitambulisho,jina na Anwani kamili ya mweka pingamizi,Number ya simu ya mkononi pamoja na nakala ya kadi ya uanachama hai,lakini pia mwekapingamizi ahakikishe anasaini rejesta ya mapingamizi kwa mpokea mapingamizi.

Kamati hiyo imesema kuwa,itaanza kusikiliza na kupitia pingamizi za wagombea siku ya tarehe 25 mwezi huu,kuanzia saa 3 hasubuhi katika viwanja vya Gymkhana Dar es salaam,ambapo watu watakaoruhusiwa kuingia katika maeneo hayo ni waweka pingamizi tu,pamoja na wagombea waliowekewa pingamizi.

Kamati itatoa maamuzi ya pingamizi siku ya tarehe 27 mwezi huu,na Usaili wa wagombea waliopita katika mapingamizi utafanyika tarehe 29 mwezi huu pia kuanzia saa 3 asubuhi katika ukumbi wa Police Officers Mess Oysterbay.

Na kamati pia imesema kuwa siku ya usahili, mgombea anatakiwa aje na nakala halisi ya vyeti vyake na picha moja ya passport size,lakini pia mgombea yeyote hataruhusiwa kuja na makundi ya mashabiki kumsindikiza katika hatua hizi za mchakato.

WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI







Post a Comment

0 Comments