Ticker

6/recent/ticker-posts

PIQUE AKUBALI KUJIFUNGIA NDANI YA BARCELONA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 21,2014 SAA 02:18 USIKU
Beki wa Barcelona Gerard Pique amekubali kutia saini
mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo ya Uhispania,ambapo walisema kwenye tovuti yao siku ya Jumanne.
Pique, 27, alipitia mfumo wa kukuza chipukizi katika klabu hiyo ya Catalona na akarejea Barca mwaka 2008 baada ya kukaa miaka minne Manchester United.
Alitekeleza jukumu muhimu katika kipindi cha ufanisi cha Barca ambapo walishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2009 na 2011 na pia wakashinda La Liga mara nne kati ya 2009 na 2013.
"Barcelona wanatangaza kwamba wamekubaliana na Gerard Pique kuongeza mkataba wake ambao ulikuwa umalizike 30 Juni 2015, kwa misimu mitano ijayo,” taarifa ya klabu hiyo ilisema.
“Mkataba huo mpya unaomuweka Barcelona hadi mwisho wa msimu wa 2018-19 utatiwa saini hivi karibuni."

Post a Comment

0 Comments