Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 21,2014 SAA 01:12 USIKU
Polisi ilibidi kuingilia kati baada ya Mario Balotelli kukabiliwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika mazoezi ya Kombe
la Dunia na timu ya Italia.
Watoto wachache nje ya uwanja wa Coverciano walihusika kufanya vitendo hivyo vya kibaguzi kwa kuimba kama nyani, na Balotelli alionekana wazi kukasirishwa na vitendo hivyo.
Kipindi cha mazoezi kulikuwa wazi kwa vyombo vya habari na Balotelli aliweza kusikika akisema, " Roma na Florence wao ni wajinga."
Wakati wengi wa mashabiki wakimshambulia Balotelli, Polisi wakakaribia eneo ambapo vilifanyika vitendo hivyo na kwa haraka wakamalizika tukio hilo.
Balotelli alizaliwa na wazazi raia wa Ghana. Kutokana na matatizo ya kiafya aliyokuwa nayo Balotelli, wazazi wake walibidi kuomba msaada kwa watu wengine ili wamlee kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kifedha.
Hivyo Balotelli akajikuta akilelewa na raia wa Italia mke na mume Francesco na Silvia Balotelli wakati huo Balotelli alikuwa na miaka tatu.Mchezaji huyo amekuwa akukabiliwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika kazi yake ya Soka.
0 Comments