Ticker

6/recent/ticker-posts

MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA NAYE ACHUKUWA FOMU YA KUGOMBEA KATIKA UCHAGUZI,ASEMA ATAKI KAMPENI

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 14,2014 SAA 10:55 ALFAJIRI
KUTOKA KULIA NI:Kamguna Khalid Aman ambaye ni katibu msaidizi wa kamati ya uchaguzi kutoka Simba,akimkabidhi fomu Abdulahamed Mshangana (Kushoto,aliyevaa tai) fomu ya kugombea ujumbe wa klabu ya Simba
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa tawi la Darajani Visiwani Zanzibar Abduhamed
Mshangama,amechukuwa fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya ujumbe wa klabu hiyo.

Mshangama ambaye ni mwenyekiti wa tawi hilo toka mwaka 2006 mpaka sasa,amesema amechukuwa fomu ya kugombea ujumbe katika klabu ya Simba ili kuweza kuleta umoja na mshikamano na maendeleo ya soka katika nchi ya Tanzania.

"kikubwa zaidi ni kuweza kuleta maendeleo,baada ya kuona wenzetu wa Azam wameleta changamoto kubwa.Uwezo wangu niliona kimpira,kwa sababu mimi mwenyewe zamani nilikuwa mchezaji wa Simba,kwaiyo nataka kuifanya Simba iende kisasa kama vili TPMazembe,kwa sababu ukiangalia kama klabu za simba na yanga zinauwezo wa kumiliki hata ndege,lakini hii leo hata ndege ya watu ishirini klabu hizi hazina,pindi nitakapochaguliwa kuwa mjumbe wa Simba nitahakikisha nashirikiana na wenzangu kufanya mabadiliko au mapinduzi ndani ya klabu ya simba"

katika hatua nyingine Mshangama amesema kuwa,yeye haitaji kampeni kwani maelezo yake atakayoyatoa katika mkutanao mkuu yatajitosheleza "Simba inapokuja Zanzibar huwa inakuwa chini ya mikono yangu kwa miaka yote ambayo niko katika madaraka,na haijawahi kupata kashfa yeyote japokuwa tumekuwa na matatizo ya hapa na pale, lakini matatizo hayo hayawezi kutoka katika vyombo vya habari" alisema Mshangama

Pia Mshangama amewaomba wanachama wote wa Simba washikamane na wawe kitu kimoja ili waweze kuijenga timu ya Simba

Post a Comment

0 Comments