Ticker

6/recent/ticker-posts

ALICHOKISEMA NAHODHA JOHN TERRY BAADA YA CHELSEA KUMPA ULAJI MPYA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 13,2014 SAA 05:44 USIKU
Nahodha wa Chelsea  John Terry amesaini mkataba mpya kwa klabu hiyo ya Stamford Bridge baada ya kukubaliana
masharti kadhaa,na amepewa mkataba wa mwaka mmoja .
Terry,amewaacha wachezaji wenzake Frank Lampard na Ashley Cole ambao bado hawajaongezewa mikataba,angali mikataba yao inamalizika msimu huu
Mchezaji huyo  mwenye umri wa miaka 33, ambaye amekuwa nahodha wa Chelsea mara 490 wakati wa kazi yake,inaeleweka kuwa awali alikuwa katika mazungumzo ya mkataba mpya na klabu hiyo ambayo  amekuwa nayo tangu akiwa na umri wa miaka 14.
Akizungumza na tovuti rasmi ya klabu, Terry alisema: "Nina furaha kusaini mkataba wangu mpya na Chelsea ambayo niko nayo kwa mwaka wangu wa 20 ".
"Ningependa kuwashukuru mashabiki na klabu kwa msaada wao unaoendelea, na meneja ambaye amekuwa mtu muhimu kwangu msimu uliopita."

Post a Comment

0 Comments