Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 11,2014 SAA 09:42 ALFAJIRI
Beki wa kushoto wa Chelsea Ashley Cole anastaafu kuitumikia timu yake ya Taifa baada ya kuachwa katika kikosi
cha England cha kocha Roy Hodgson kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu.
cha England cha kocha Roy Hodgson kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu.
Roy Hodgson alimpigia simu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 , ambaye amecheza mechi 107 , kumjulisha kwamba yeye hajajumuishwa katika safari hiyo ya ndege, na mchezaji wa Southampton Luka Shaw amechukuwa nafasi yake.
Mchezaji huyo wa Southampton mwenye umri wa miaka 18 Luka Shaw ameitwa na Hodgson, pamoja na Leighton Baines.
Ashley Cole ali tweete: "nimepokea simu kutoka kwa Roy na kukukubaliana kwamba kikosi cha England lazima kihusishe wachezaji vijana. Nadhani sasa ni bora nistaafu katika timu ya Uingereza".
"Tuna meneja mkubwa na timu na Ninawatakia mafanikio tu.Mimi nitakuwa nawasaidia kama shabiki wa kweli. Shukrani kwa kila mtu na kwa kila kitu,kwa anayenipenda na asiyenipenda, kiukweli imeniuma kuacha kuichezea nchi yangu"
"Baines na Shaw ni wachezaji wakubwa, wameonekana msimu huu, na ni tegemeo la baadaye la nchi hii, ilikuwa ni furaha kucheza mechi 107 "aliandika Ashley Cole
Kuwapa vijana nafasi: Roy Hodgson amerejesha vijana katika kikosi cha England katika orodha ya majina ya kwenda katika Kombe la Dunia
|
Ametwa: kijana wa Everton Ross Barkely naye pia yuko katika kikosi
Wanakabiliwa na shoka: wachezaji wa Manchester United Michael Carrick (kushoto) na Ashley Young wanatarajiwa kukosa katika kikosi
|
Hatari: mchezaji wa Arsenal Oxlade-Chamberlain (hapo juu) na Jack Wilshere (chini) wote wawili wanasemekana kuwepo licha ya matatizo yao ya kuumia.
|
Moto wa nguvu :Hodgson atasimama upande wa Rickie Lambert, ambaye alikuwa ni sehemu muhimu katika kampeni ya kufuzu?
|
Vyanzo mbalimbali vya habari vinaripoti kuwa kiungo wa Manchester United Michael Carrick na beki wa Tottenham Kyle Walker pia wamekosa katika orodha hiyo ya Hodgson itakayotolewa Jumatatu mchana.
Phil Jones (22), Jordan Henderson (23), Jack Wilshere (22), Raheem Sterling (19), Alex Oxlade-Chamberlain (20), Danny Welbeck (23), Barkley (20) na Shaw wote wameitwa katika safari hiyo kwa ajili ya Brazil inavyosemekana.
Atapuuzwa: mshambuliaji wa Toronto FC Jermain Defoe atakuwepo?
|
Imewekewa nafasi yake?: Phil Jones akishika bega lake aliloumia |
Naye meneja wa England Roy Hodgson amekubali kushindwa kumtaja Ashley Cole kwa ajili ya kikosi cha Kombe la Dunia na akisema kuwa ilikuwa "ni moja ya maamuzi magumu" katika kazi yake.
Bosi huyo wa zamani wa West Brom amebaini kuwa ameumia kwa kiasi kikubwa juu ya uamuzi wa kuwachukua Luka Shaw na Leighton Baines badala ya Cole .
"Miongoni mwa maamuzi yangu magumu ambayo nimepata kuyafanya kwa ajili ya kikosi changu, ni kutomchagua Ashley ilikuwa ni moja ya maamuzi magumu," Hodgson aliiambiaTheFA.com.
0 Comments