Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 11,2014 SAA 10:42 JIONI
Meneja wa England Roy Hodgson amemteua kijana wa Everton Ross Barkley katika kikosi chake cha wachezaji 23
kwa ajili ya Kombe la Brazil Dunia.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 ni mmoja wa wachezaji wanane wa chini ya umri wa miaka 24 alithibitishwa kuwa katika kundi moja na Luka Shaw (18), Raheem Sterling (19), Alex Oxlade-Chamberlain (20), Phil Jones (22), Jack Wilshere (22), Jordan Henderson (23) na Danny Welbeck (23).
Hodgson, ambaye ametangaza rasmi kikosi chake pia alithibitisha kuwa wa wachezaji wazoefu wa kimataifa Wayne Rooney, Steven Gerrard, Frank Lampard, James Milner, Joe Hart na Glen Johnson wate wapo katika kikosi hiko.
Kikosi hiko kimetangazwa siku moja baada ya Beki wa kushoto wa Chelsea Ashley Cole kutangaza anastaafu kuitumikia timu yake ya Taifa baada ya kuachwa katika kikosi hiko cha England cha kocha Roy Hodgson kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu.
Roy Hodgson alimpigia simu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 , ambaye amecheza mechi 107 , na kumjulisha kwamba yeye hajajumuishwa katika safari hiyo ya ndege, na mchezaji wa Southampton Luka Shaw amechukuwa nafasi yake.
Ashley Cole aliweka ujumbe katika mtandao wa twitter akisema: "nimepokea simu kutoka kwa Roy na kukukubaliana kwamba kikosi cha England lazima kihusishe wachezaji vijana. Nadhani sasa ni bora nistaafu katika timu ya Uingereza".
"Tuna meneja mkubwa na timu na Ninawatakia mafanikio tu.Mimi nitakuwa nawasaidia kama shabiki wa kweli. Shukrani kwa kila mtu na kwa kila kitu,kwa anayenipenda na asiyenipenda, kiukweli imeniuma kuacha kuichezea nchi yangu"
"Baines na Shaw ni wachezaji wakubwa, wameonekana msimu huu, na ni tegemeo la baadaye la nchi hii, ilikuwa ni furaha kucheza mechi 107 "aliandika Ashley Cole
Naye Hodgson alikubali kuwa kushindwa kumtaja Ashley Cole kwa ajili ya kikosi cha Kombe la Dunia na akisema kuwa ilikuwa "ni moja ya maamuzi magumu" katika kazi yake.
Naye Hodgson alikubali kuwa kushindwa kumtaja Ashley Cole kwa ajili ya kikosi cha Kombe la Dunia na akisema kuwa ilikuwa "ni moja ya maamuzi magumu" katika kazi yake.
Full squad: Joe Hart (Man City), Ben Foster (West Brom), Frasier Forster; Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Man Utd), Phil Jagielka (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Man Utd), Leighton Baines (Everton), Luke Shaw (Southampton); Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Southampton), Raheem Sterling (Liverpool), Steven Gerrard (Liverpool), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Man City), Ross Barkley (Everton); Wayne Rooney (Man Utd), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Man Utd), Rickie Lambert (Southampton)
Stand-bys: John Ruddy (Norwich) John Flanagan (Liverpool), John Stones (Everton), Michael Carrick (Man Utd), Jermain Defoe (Toronto), Andy Carroll (West Ham), Tom Cleverley (Man Utd)
0 Comments