Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:ANGALIA KILICHOTOKEA UWANJA WA TAIFA BAADA YA WATU KUTANGAZIWA KUINGIA BURE KATIKA MECHI YA STARS NA BURUNDI

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 27,2014 SAA 01:51 USIKU

Siku ya jana timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilishindwa kuwapa raha watanzania walikuwa wakisherehekea sherehe za miaka 50 za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa timu
ya Burundi (Intamba Mu Rugamba) katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopingwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Lakini kama utakuwa na kumbukumbu vizuri kabla ya mchezo huo kulitangazwa kwa viingili vya kuangalia mtanange huo,lakini mambo yakabadilika mara baada ya mmoja wa viongozi wa serikali ambaye alikuwa katika uwanja wa uhuru ilioko karibu kabisa na uwanja uliokuwa unatakiwa kupigwa kwa mechi hiyo, alitangaza kuwa watu wote wanaweza kwenda kuangalia mchezo kati ya Tanzania na Burundi Bure kabisa.
Mashabiki wa mpira wakoinesha Tiketi walizokata
Ndipo kulipotokea hali ya kutokuwelewana kati ya mashabiki ambao walilipa pesa zao na uongozi wa uliokuwa unaosimamia mchezo huo,kwani mashabiki hao walitaka kurudishiwa pesa zao.


Mashabiki hao walichukua hatua ya kuandamana kwa kutembea uwanjani humo huku wakipinga kitendo hiko cha kuwaruhusu watu wengine kuingia bure,lakini mwisho wa siku hawakurudishiwa pesa zao.

Katika hatua nyingine ndani ya mchezo huo uliokuwa ukipigwa katika uwanja wa Taifa,baadhi ya mashabiki wa tanzania walikuwa wakiishangilia timu ya Burundi hata mara baada ya kufunga goli.
Mtanzania akiwa na Jezi ya Tanzania lakini akishangilia Burundi

Mchezo huo ulikuwa niwakujipima nguvu kwa timu ya Tanzania ambayo ilikuwa ikisheherekea miaka 50 za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

PICHA NYINGINE ZA MATUKIO MBALIMBALI


Kikosi cha  timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars


Kikosi cha timu ya Burundi (Intamba Mu Rugamba)
Wambele ni Rais wa Shirikisho la Soka Burundi (FFBReverien Ndikuriyo akiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wakikagua timu kabla ya mchezo.




Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akimfariji beki wa Azam FC,Samih Haji Nuhu kabla ya mchezo wa jana wa kirafiki wa kimataifa kati ya Tanzania na Burundi.Beki huyo wa Azam FC amerejea hivi karibuni kutoka nchiniAfrika Kusini kufanyiwa upasuaji wa goti.




 Kocha Salum Mayanga
Kocha wa Burundi (Intamba Mu Rugamba) Niyungeko Alain Olivier,akizungumza baada ya mechi.

Kocha Salum Mayanga akizungumza baada ya mchezo.


Post a Comment

0 Comments