Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:ANGALIA YANGA ILIVYOPAMBANA NA AL AHLY LEO TAIFA

Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Young Africans,wameibuka na
ushindi wa bao 1 kwa 0 katika mchezo dhidi ya Al Ahly uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Bao pekee la Naodha wa timu ya Young Africans Nadir Haroub "Cannavaro"katika dakika ya 82 ya mchezo,liliweza kuwainua vitini mashabiki wa timu hiyo na kuweza kuwanyamazisha mashabiki wachache wa timu ya Al Ahly ambao walijichanganya na wapinzani wa Yanga kwa Tanzani.
Washambuliaji wa Young Africans walikosa nafasi zaidi ya nne kipindi cha kwanza kutokana na kutokua makini na kukuta mashuti yao yakiokolewa na walinzi wa Ah Ahly na mlinda mlango wao Sherif Ekramny.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Al Ahly.



Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko kuhakikisha wanapata mabao ya mapema lakini mabadiliko hayo yaliisadia Young Africans zaidi kuweza kumiliki mchezo na kutawala eneo la ulinzi.
 Dakika ya 82  kona iliyopigwa na Saimon Msuva ilitua kichwani kwa Nahodha Nadir Haroub "Cannavaro" na kuukwamisha wavuni na kuwaacha mabingwa watetezi Al Ahly na benchi la Ufundi wakiduwaa.


Post a Comment

0 Comments