Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 15,2014 SAA 02:27 USIKU
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imeendelea leoo (Machi 15 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo mabingwa watetezi Yanga
walikuwa wakiumana na Mtibwa Sugar kwenye
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Katika mchezo huoo,timu ya zote mbili ziimeechoshana nguvu kwa kutokaa sare ya bila kufungana,ingawa Mtibwa Sugar walimaliza pungufu kwa mchezaji wao Abdala Juma kupewa kadi nyekundu
Nao vinara wa ligi hiyo, Azam
walikuwa wakiwakaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi iliyofanyika katika Uwanja wa
Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam,na katika mchezo huo Azam Fc imeibuka na ushindi wa mabao 4 kwa 0.
Mabao mawili ya Kipre Herman Tchetche katika dakika ya 21 na 38,pamoja na John Raphael Bocco ‘Adebayor’ katika dakika ya 64,na mshambuliaji aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili, Kevin Friday alipachika bao la nne la Azam FC na kuhitimisha ushindi huo mnono kabisa.
Mechi nyingine ilichezwa Uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba kwa kuwakutanisha wenyeji Kagera Sugar dhidi ya maafande
wa Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya,na Kagera sugar wakaibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1.
Mabao ya Kagera Sugar yakifungwa na Salum Kadoni na Benjamini Asukile, huku kwa upande wa Tanzania Prisons bao lao pekee likiwekwa nyavuni na Peter Michael.

0 Comments