Ticker

6/recent/ticker-posts

HUU NDIO UAMUZI ALIOAMUA JOSE MOURINHO BAADA YA MWAMUZI FOY KUWATOA NJE WACHEZAJI WAKE WAWILI

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 17,2014 SAA 02:39 USIKU

Kocha Jose Mourinho ametoa wito kwa viongozi wa Ligi Kuu 
kuacha kumtuma mwamuzi Chris Foy katika michezo ya Chelsea baada ya mwamuzi huyo kuwatoa nje kwa kadi nyekundu wachezaji wawili wa Chelsea katika mchezo ambao walifunga bao 1-0 na Aston Villa siku ya Jumamosi.

Foy alimtoa WILLIAN kwa kadi ya pili ya njano katika uwanja wa Villa Park kabla ya kumtoa Ramires katika dakika za mwisho wa mchezo baada ya kukabiliana na Karim El Ahmadi.

Meneja wa Chelsea Mourinho akaja juu ya uwanja baada ya kadi ya pili nyekundu na pia kupelekwa nje na  mwamuzi Foy, ambaye hakutaka kuzungumza na kocha huyo wa Kireno baada ya mchezo. 

Mourinho alionesha ubora wake katika kuumba maneno  baada ya mechi katika mkutano na vyombo vya habari , "Labda ni kusaidia  ( Mwamuzi wa Ligi Kuu ') Kamati isimpeleke (Foy) kwenye mechi zetu," alisema Mourinho.

"Sina haki ya kuomba (hili) nadhani nimechambua hali na kuona kuwa kila wakati akiwa na Chelsea -. au si kila wakati - lakini mara nyingi akiwa na Chelsea  matatizo yako pale, mimi nafikiri labda itakuwa ni uamuzi mzuri. "alisema Mourinho

Ingawa hakuwa meneja, Mourinho alikumbuka Chelsea iliposhindwa na QPR katika mwaka 2011 wakati Foy lipowatoa nje Jose Bosingwa na Didier Drogba. 

 

Post a Comment

0 Comments