Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 20,2014 SAA 11:56 JIONI
Meneja wa Everton Roberto Martinez imekataa taarifa kuwa Manchester United iko katika mazungumzo ya kumasaini mlinzi wa
klabu hiyo, Seamus Coleman.
Mlinzi huyo wa Jamhuri
ya Ireland amekuwa akitolewa macho katika msimu huu,kufuatia utendaji wake wa kazi katika kikosi cha Evarton , na mkataba wake na timu hiyo ya Goodison Park bado unaendelea hadi Juni 2018.
Hata
hivyo, Meneja wa United David Moyes ameripotiwa kuwa na nia ya kumleta mchezaji huyo mwenye miaka 25 ndani ya Old Trafford katika majira ya joto, lakini Mhispania Martinez ameweka ngumu ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayeweza kuwasiliana na kujadili juu ya mchezaji huyo anayemtegemea katika
siku zijazo.
Alisema: "Ni lazima kuwe na tofauti kwa Seamus Coleman kwa sababu sisi hatujawai kuwa na majadiliano yoyote na mtu yeyote".
"Nadhani
ukweli ni kwamba Seamus amekuwa na msimu mzuri sana na tunataka kuendelea na tunamatumaini katika kipindi cha michezo 10, anaweza
kuendelea na kiwango cha juu kwani ameonyesha na bado anaendelea". alisema Roberto Martinez
0 Comments