Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 20,2014 SAA 11:56 JIONI
Mshambuliaji
wa Kimataifa wa Nigeria, Peter Odemwingie ameelezea wasiwasi wake wa kama ataweza
kuwa katika kikosi
cha Nigeria katika fainali za Fifa za Kombe la Dunia nchini
Brazil mwaka huu 2014 .
Hii ni kulingana na mchezaji mwenzake katika Ligi kuu ya Uiingereza katika klabu ya Stoke City, Asmir Begovic.
Begovic ambaye ana kofia 28 kwa timu yake ya taifa Bosnia-Herzegovina anaweza kukutana
na Odemwingie wakati wa timu ya Ulaya itakapokutana na Nigeria Super Eagles katika kombe la dunia 2014 Juni 14 katika uwanja Pantanal, Cuiaba.
Odemwingie hakuwa mchezaji katika kikosi cha Nigeria tangu Februari 29, 2012 katika Kombe la
mataifa ya Afrika katika mchezo wa kufuzu dhidi ya Rwanda huko Kigali.
Bergovic sasa amebaini kuwa Odemwingie hajui kama yeye atakuwa pamoja na Stephen Keshi katika kikosi cha kombe la dunia la FIFA 2014.
"Mimi na Peter tumekuwa na mazoezi kila siku.
Yeye hana uhakika kabisa wa kwenda katika kikosi bado na sisi sote huwa tunaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha tunapata nafasi ya kwenda Brazil".
0 Comments