Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 13,2014 SAA 11:O JIONI
Beki wa Manchester
City Pablo Zabaleta amemshutumu mwamuzi wa Kifaransa Stephane
Lannoy kwa kumkosoa mwamuzi huyo
kuwa "alifanya maamuzi ya kutisha" kwa Manchester
City ambayo walifungwa mabao 2-1 na Barcelona.
Mlinzi huyo wa Argentina,Zabaleta alitolewa nje katika uwanja wa Nou Camp kwa kadi ya nyekundu baada ya kumzonga mwamuzi
Lannoy kwa sababu ya kushindwa kutoa adhabu wakati Edin Džeko
alipoonekana kufanyiwa madhambi na Gerard Pique ndani ya boksi.
Zabaleta
mara baada ya kusisitiza kwamba City lazima wapewe Penalti baada ya Džeko kufanyiwa tukio hilo,
na anadai kuwa yeye bado yuko katika sintofahamu ya kwa nini alitolewa nje kwa kadi hiyo ya pili ya njano.
"ilikuwa ni wazi sana," Zabaleta alisema. "Nadhani Pique alikuwa nyuma yangu na alifanya kukabiliana na Džeko na mwamuzi alikuwa mita mbili tu kutoka umbali".
"sijui ni kwa nini alinitoa mimi wakati nilikwenda kwake kuzungumza naye kwa njia nzuri".
"kidogo nilikuwa na hasira kwa sababu yeye hakutoa adhabu, lakini mimi nimekuwa na heshima sana kwake".
"Nilichanganyikiwa. Nadhani ni uamuzi wa kutisha".

0 Comments